Rais wa Marekani, Donald Trump, ametoa matumaini makubwa kwa ulimwengu, akisema mkataba wa amani wa kumaliza vita kati ya Urusi na Ukraine unaweza kufikiwa na kutekelezwa katika siku za usoni. Kauli hii aliitoa baada ya kukutana na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, na viongozi wengine wa Ulaya, ambapo alisisitiza kuwa suluhisho linaweza kupatikana kwa masuala yote, ikiwemo masuala muhimu ya kiusalama.
Katika mkutano huo uliofanyika Ikulu ya Marekani (White House), Trump alielezea matumaini yake kwamba, kwa ushirikiano wa Ulaya, wataweza kufikia makubaliano yatakayozuia Urusi kuishambulia Ukraine tena siku zijazo. Alisema Marekani na Ulaya watachukua jukumu muhimu la kusaidia Ukraine na kuihakikishia usalama wake.
Trump pia aligusia suala tata la kubadilishana maeneo ya ardhi, akisema kuna haja ya kujadili suala hili kwa kuzingatia hali halisi ya mstari wa sasa wa mapigano (contact line). Alisema anahisi kwamba kuna uwezekano wa kufanyika mazungumzo ya pande tatu, yatakayohusisha yeye, Rais Zelensky, na Rais wa Urusi, Vladimir Putin, na kwamba mazungumzo hayo yanaweza kuzaa matunda ya amani.
Kama sehemu ya mkataba huu, inadhaniwa kuwa Ukraine inaweza kutopewa uanachama wa NATO, lakini badala yake itahakikishiwa msaada wa kijeshi wa moja kwa moja kutoka kwa washirika wake wa Ulaya na Marekani endapo itashambuliwa tena. Hii inafanana na Kifungu cha 5 cha mkataba wa NATO, ambacho kinaeleza kuwa shambulio kwa mwanachama mmoja ni shambulio kwa wote. Trump alidokeza kuwa Putin amekubali makubaliano haya.
Kwa upande wa Urusi, imeripotiwa kuwa Putin alimuomba Trump kuwa Urusi inyeke nyara eneo la Donbass, ambalo linajumuisha majimbo ya Donetsk na Luhansk. Kama Ukraine itakubali kuachia maeneo hayo, Urusi inasemekana kuwa itasimamisha mapigano na haitafanya mashambulizi zaidi kusini mwa nchi hiyo.
Rais Zelensky alionyesha shukrani zake kwa Trump na viongozi wa Ulaya kwa uungwaji mkono wao. Ingawa awali alikuwa akikataa kata kata suala la kurudisha maeneo ya ardhi, Zelensky alibadilisha msimamo wake na kusema kuwa masuala hayo nyeti, ikiwemo ya ardhi, yanaweza kujadiliwa kwenye mazungumzo ya pande tatu. Alisema Ukraine itakubali kwa furaha ushiriki katika mkutano huo.
Baada ya kumaliza mkutano na viongozi wa Ulaya, Trump alipanga kumpigia simu Rais Putin ili kumweleza matokeo ya mazungumzo yao.