Msiba umetokea katika eneo la magharibi mwa Urusi, mkoa wa Bryansk, ambapo daraja limeporomoka na kusababisha vifo vya watu wasiopungua saba.
Shirika la habari la Urusi la TASS liliripoti kuwa tukio hilo lilitokea takriban saa kumi na moja jioni kwa saa za huko (saa tano usiku kwa saa za Afrika Mashariki) tarehe 31, wakati daraja moja huko Bryansk lilipopomoka na kusababisha treni iliyokuwa ikisafiri kutoka Moscow kupita eneo hilo kutoka reli.
Mamlaka ya reli ya Moscow ilitoa taarifa ikisema kuwa "daraja liliharibiwa kutokana na kitendo haramu," na kwamba uchunguzi umeanzishwa ili kubaini mazingira kamili ya ajali hiyo.