Google Yaamsha 'Dude' Jipya: 'Gemini 3 Deep Think' Yatua kwa Kishindo, Yampiga 'Gap' la Ajabu GPT-5

it | Mon Dec 08 2025


Google Yaamsha 'Dude' Jipya: 'Gemini 3 Deep Think' Yatua kwa Kishindo, Yampiga 'Gap' la Ajabu GPT-5

Hatimaye Google imevunja ukimya na kuleta mapinduzi ambayo yameacha ulimwengu wa teknolojia mdomo wazi. Katika kile kinachoonekana kama kuitwaa taji la "Mfalme wa Akili," kampuni hiyo imezindua mtambo mpya wa Akili Mnemba (AI) uitwao ‘Gemini 3 Deep Think’.


Tofauti na maroboti tuliyozoea ambayo hujibu maswali haraka haraka (kama mtu anayekariri), mtambo huu mpya umeundwa "Kufikiri kwa Kina" (Reasoning) kama mwanasayansi au mtaalamu wa hisabati ngazi ya PhD. Tangazo hili la Jumatano (Desemba 4) limekuja na bei ya "kichetamkwa" ya Dola 250 kwa mwezi (Takriban Shilingi 675,000 za Kitanzania), ikiashiria kuwa hii si bidhaa ya mchezo.


Akili ya "Parallel Reasoning": Kufikiri Njia Nyingi kwa Mpigo


Siri ya uwezo wa Gemini 3 Deep Think ni teknolojia mpya inayoitwa "Advanced Parallel Reasoning."


Jeff Dean, Mwanasayansi Mkuu wa Google, amefafanua kuwa tofauti na AI za kawaida zinazofikiri mstari mmoja (Hatua A kwenda B), mtambo huu unachunguza "Dhana Nyingi kwa Wakati Mmoja." Ni kama mchezaji wa Chess anayefikiria hatua 10 mbele kwa njia tofauti kabla ya kusogeza kete.


Mtambo huu ni toleo lililoboreshwa la ‘Gemini 2.5 Deep Think’ ambayo iliwahi kushinda medali za dhahabu katika mashindano ya kimataifa ya hisabati (IMO). Unatumia mbinu ya "Reinforcement Learning" (Kujifunza kwa Tuzo) ili kuhakikisha jibu lina mantiki iliyonyooka.

Vipimo vya Ufaulu: Google Yavunja Rekodi Zote


Katika ulimwengu wa AI, ubora hupimwa kwa mitihani migumu (Benchmarks). Matokeo ya Gemini 3 Deep Think yamevunja rekodi ambazo zilionekana kutosogeleka.


Mtihani (Benchmark)Gemini 3 Deep ThinkGemini 3 ProGPT-5 Pro (OpenAI)Claude Sonnet 4.5
HLE (Humanity's Last Exam)41%37.5%30.7%13.7%
ARC-AGI-2 (Akili ya Ujumla)45.1%31.1%(Chini ya 20%)N/A
GPQA Diamond (Sayansi ya PhD)93.8%N/AN/AN/A


Matokeo haya yanaonyesha kuwa Google sasa imeiacha mbali GPT-5 ya OpenAI na Claude ya Anthropic, hasa katika maswali yanayohitaji akili ya utatuzi (Reasoning) badala ya kukariri.


Gharama ya Akili: "Kufikiri Kunagharimu Pesa"


Hata hivyo, akili hii ina gharama kubwa sana. Imebainika kuwa mtambo huu unatumia nguvu kubwa ya kompyuta (Compute Power) kufikiria.


Taasisi ya ARC Prize imetoa mfano wa kushangaza:

  1. Kutatua swali moja gumu kwa kutumia Gemini 3 Pro kuligharimu Dola 0.81 (Tsh 2,100).
  2. Kutatua swali hilo hilo kwa Gemini 3 Deep Think kuligharimu Dola 77.16 (Tsh 208,000)!


Hii ni tofauti ya mara 100 ya gharama. Hii ndiyo sababu huduma hii inauzwa kwa bei mbaya ya Dola 250 kwa mwezi, na inalenga wataalamu wa juu, watafiti, na makampuni makubwa, siyo mtumiaji wa kawaida wa Instagram.


OpenAI Hatarini Kupoteza Taji


Wachambuzi wa soko wanasema uzinduzi huu ni "Kengele ya Hatari" kwa OpenAI. Kwa muda mrefu, OpenAI ndiyo ilikuwa ikishikilia taji la "Reasoning" (Uwezo wa kufikiri), lakini sasa Google imeipokonya taji hilo rasmi.


"Sasa hatuangalii tu ukubwa wa data, tunaangalia nguvu ya kufikiri wakati wa kujibu (Inference-time compute)," alisema mchambuzi mmoja. "Kama OpenAI haitatoa kitu kipya haraka, watapoteza ufalme wao."


Kwa sasa, mtambo huu unapatikana kwenye App ya Gemini pekee, ingawa kuna tetesi kuwa Google inafikiria kuurusu kwa wasanidi programu (API) hivi karibuni, jambo litakalofungua ukurasa mpya wa programu zenye akili ya kiwango cha PhD.

The copyright for this content belongs to the copyright holder or provider. Unauthorized use may result in legal liability under copyright laws and other regulations.