Ndoa ya Haji Manara na Zaylissa Yatumbukia Shimoni, Talaka Yawadia

culture | Thu Apr 10 2025


Ndoa ya Haji Manara na Zaylissa Yatumbukia Shimoni, Talaka Yawadia

Ufuatiliaji wa karibu wa mitandao ya kijamii, hususan Instagram, kuanzia Aprili 9, 2025, unaacha maswali mengi kuhusu hatima ya ndoa iliyokuwa gumzo kati ya Haji Manara, msemaji maarufu, na Zaylissa, muigizaji wa tamthilia ya Jua Kali na mwanamitindo. Ndoa yao, ambayo ilitimiza mwaka mmoja hivi karibuni, inaonekana kuwa katika hali tete baada ya wawili hao kurushiana maneno makali kwenye mitandao ya kijamii.


Zaylissa ameonekana akilalamika kwa muda mrefu kuhusu tabia za Manara, akidai kuwa ameshindwa kuzivumilia na hivyo kuomba talaka mara kadhaa bila mafanikio. Ujumbe wake aliouchapisha unaonesha hisia kali za kukata tamaa na madai mazito.


"Mtu Mzima ovyo ww, m.......zi mkubwa Imetosha Sasa nimechoka kupretend...Sasa Acha tuvuane nguo Kama ulivyozoea. Mtoto wa dada Angu amekuja kukaa likizo kwa mapenzi na muda wake wa kuondoka ulivyofika ulimzuia! Kumbe ulikuwa unamtongoza shame on you Ulikuwa na kazi ya kumshika shika m…..wa binti mdogo wa under 18! Sasa round hii umechezea pabaya Umezoea kulala ma house girl Sasa ukaona uhamie kwa binti yangu loh. Unamtumia mtoto vi 50k vyako Akiwa shule ili umlaghai Kwa taarifa yako tuna ushahidi wote! Na driver wako pia anajua kila kitu na tumeambiwa na hatutakukalia kimya Kila nikiomba talaka yangu hutaki kunipa jina…zi we Unagombana na Mimi unamwambia kijana wako arecord Kisha unaongea vya uongo! Unantishia kupeleka kwa mange ili unidhalilishe...Sasa round hii sicheki na kima Kama ushazoea kudhalilishana Ntakupa unachostahili,” aliandika Zaylissa kwa hasira.


Hata hivyo, Haji Manara alijibu madai hayo kwa maneno mafupi yaliyoonekana kudharau hali hiyo.


"Umekuja hata nguo huna ya kuvaa Leo unasema jogoo wangu hapandi mtungi! Unawanyima wanangu chakula. Bora watu waseme naoa sana ,Wacha aende tu.." aliandika Manara.


Katika chapisho lingine lililoonekana kuwa na hisia kali zaidi, Manara aliweka wazi kuwa familia yake ndio kipaumbele chake.


"Mama yangu na Baba yangu na Watoto wangu wapo juu ya kila kitu duniani kasoro Mungu tu.,,Heri nisemwe naoa sana lakini Mwanangu hadi kunyimwa chakula nnachokihangaikia baba yake kwa jasho jingi,,sikubali abadan,,Mtanisamehe Waja wa Manani 🙏🙏AENDE TU," aliandika Manara, akionyesha kuwa yuko tayari kumwacha Zaylissa aende zake.


Baada ya uvumi kuenea kuwa Zaylissa amepokea talaka yake, alichapisha ujumbe kwenye mtandao wake akishukuru kwa kuongozwa kutoka kwenye giza hadi kwenye nuru. Alieleza kuwa ulikuwa uamuzi mgumu lakini anasimama imara zaidi na ana matumaini kuhusu maisha yake ya baadaye kama mshawishi wa chapa.


"Thanking God for guiding me out of darkness and into the light. It was the hardest decision, but today, I stand stronger and more determined than ever. I’m excited and blessed to be working with incredible brands as a brand influencer, a path I’m embracing with open arms. Remember, healing is possible, and your past does not define your future. Keep moving forward," aliandika Zaylissa.


Alipotafutwa Haji Manara kuzungumzia suala la talaka, alikataa kuzungumza zaidi ya kusema kuwa chapisho lake la awali la "AENDE TU" linatosha. "No comment post niliyoweka inatosha," alifupisha Manara.


Wakati hayo yakiendelea, msanii wa muziki wa singeli, Dulla Makabila, ambaye pia aliwahi kuwa mume wa Zaylissa, alichapisha picha yake akiwa studio. Akifuatana na mdundo wa muziki wa huzuni, aliwauliza mashabiki wake ni muda gani wanataka wimbo wake mpya utoke, "MNATAKA SAA NGAPI ?". Hii imeongeza udadisi wa watu kuhusu uhusiano wake na Zaylissa na kama anaweza kuwa anatoa wimbo unaohusiana na hali hiyo.


Sakata hili limekuwa likifuatiliwa kwa karibu na mashabiki na watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini Tanzania, huku kila upande ukitoa maoni yake kuhusu chanzo na hatima ya ndoa hii iliyoonekana kuwa na matumaini hapo awali.


I recommend this article.

You can participate in article recommendations up to 50 times within 24 hours.


0 comments


Messages unrelated about this certain topic may be deleted or restricted.

0/300
Loading...

The copyright for this content belongs to the copyright holder or provider. Unauthorized use may result in legal liability under copyright laws and other regulations.