Mashujaa Waliosahaulika wa Vita vya Kagera Wamlilia Rais Samia

culture | Tue Jul 08 2025


Mashujaa Waliosahaulika wa Vita vya Kagera Wamlilia Rais Samia

Wakongwe wa Jeshi la Mgambo walioshiriki bega kwa bega na Jeshi la Wananchi (JWTZ) katika Vita vya Kagera (1978-79) wametoa kilio chao kwa Rais Samia Suluhu Hassan, wakiomba waangaliwe kwa jicho la huruma na kuingizwa kwenye mpango wa pensheni na kifuta jasho. Wanajeshi hawa wa zamani wanasema licha ya mchango wao katika kulinda nchi, wamesahaulika na sasa wanaishi maisha ya dhiki.


Ombi lao limepata nguvu mpya kufuatia tangazo la hivi karibuni la serikali, kupitia kwa Waziri wa Ulinzi, Dkt. Stergomena Tax, kwamba maveterani wa JWTZ walioshiriki vita hiyo wataanza kulipwa pensheni kuanzia Julai 2026. Hali hii imewapa matumaini lakini pia imewaibua swali, "Je, vipi kuhusu sisi?"


Miongoni mwao ni Vaileth Lukonge (64), mkazi wa Mafiga, Morogoro, ambaye alijiunga na Jeshi la Mgambo mwaka 1977. "Niliitumikia nchi yangu kwa moyo wote. Ingawa sikufanikiwa kuajiriwa jeshini kwa sababu ya mazingira magumu, nilishiriki katika ulinzi. Lakini leo, sina stahiki yoyote, naishi maisha ya shida," anasema Mzee Lukonge kwa masikitiko.


Naye Ally Salumu Mbiki (69), mkazi wa Morogoro, anaeleza jinsi alivyokuwa mkufunzi wa askari wa FFU wakati wa vita, akiwafundisha mbinu za mapigano kabla ya kwenda mstari wa mbele. "Baada ya vita, nilipata tu fulana yenye maandishi ‘ahsanteni wanajeshi wetu’. Hakuna kifuta jasho, hakuna pensheni. Nimezeekea kwenye shida huku afya ikizorota," anasema Mzee Mbiki.


Wazee hawa wanasema hawapingi wenzao wa JWTZ kupata haki yao, bali wanaomba na wao, kama sehemu ya mashujaa wa operesheni hiyo ya kihistoria, watambuliwe na kusaidiwa ili waishi maisha ya utu na heshima katika umri wao wa uzeeni. Matumaini yao yote sasa yapo kwa Rais Samia, wakiamini sauti zao zitasikika na kupata suluhu.

I recommend this article.

You can participate in article recommendations up to 50 times within 24 hours.


0 comments


Messages unrelated about this certain topic may be deleted or restricted.

0/300
Loading...

The copyright for this content belongs to the copyright holder or provider. Unauthorized use may result in legal liability under copyright laws and other regulations.